Thursday, November 7, 2013

MAOMBI YAMRUDISHA BINTI WA MIAKA 16 KUTOKA ZIWA TANGANYIKA - UFUFUO NA UZIMA KIGOMA


Binti Maria John alifikishwa kanisani Ufufuo na Uzima - Kigoma akiwa hoi huku hajitambui. Bila kukawia wapiganaji wazuri kabisa wa kanisa la Ufufuo na Uzima - Kigoma walianza kumuombea binti huyu. 


Maria akiwa hajitambui wakati anaombewa.

Wakati wachungaji wanaendelea kumuombea, timu ya taarifa ilipata nafasi ya kuongea na wazazi wake ili kujua kilichojiri na kumsibu mwanafunzi huyo. Wazazi wake walidai kuwa binti yao ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Kitwe hapa Kigoma, na ana umri wa miaka 16. 




Kwa mujibu wa wazazi wake, Tatizo hilo lilimuanza ghafla baada ya kuanza kusikia kizunguzungu akiwa darasani na palepale hali ilibadilika na kupoteza fahamu ndipo walipoamua kumuwahisha Kanisani Ufufuo na Uzima Kigoma kwa maombezi zaidi.


Baada ya muda binti akafunguliwa na kusimulia kuwa alikuwa katika ziwa Tanganyika huku amefungwa minyoror mikono na miguu. Sasa Maria karudi kwenye mwili wake, ni mzima na minyororo hiyo ilikatika baada ya kusikia sauti inamuita "Maria njoooooooooooooo"

1 comment: