Tuesday, October 29, 2013

MATENDO MAKUU AMBAYO MUNGU AMEYATENDA KUPITIA KWA MCHUNGAJI KIONGOZI, JOSEPHAT GWAJIMA WA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA, MJINI MOSHI


USHUHUDA WA MAGRETH
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima, akimuombea Magreth afunguliwe dhidi ya vifungo vya shetani vya magonjwa.


Magreth akiuelezea umati wa watu katika viwanja vya mashujaa mjini Moshi kuhusiana na tatizo alilokuwa anasumbuliwa nalo na akielezea kupona kwake.


    Magreth aliyekuwa akisumbuliwa na tatizo la maumivu makali ya tumbo na pia kutokwa na damu (bleeding) kwa muda mrefu sana. Anaitwa MAGRETH, aliyeshuhudia kuwa baada ya kuhudhuria mkutano katika viwanja vya mashujaa amepona kabisa baada ya kuombewa na Mchungaji Josephat Gwajima, amepokea uponyaji wake wa tumbo na damu zime acha kabisa kumtoka kwa jina la yesu. Anamshukuru Yesu kwa kumponya.


USHUHUDA WA SARAH


         Binti huyu hapa juu anaitwa SARAH, mkazi wa Moshi mjini, alichukuliwa msukuleni na baba mkwe wake na kumpeleka Singida kulima mashamba ya mahindi na alizeti. Binti huyu alionekana kuchoka sana mara baada ya kurudishwa toka  msukuleni,jambo lililosababishwa na ugomvi uliotokea kati yake na babamkwe wake. Sarah aliendelea kushuhudia kuwa mara baada ya kuanza kuita watu wote waliochukuliwa misukule NJOOO KWA JINA LA YESU, gafla kulitokea ugomvi huko alikokuwa amefungiwa  hadi kujeruhiwa katika mkono wake wa kulia. Binti huyu  alionekana mwenye kuvimba sana mkono wake wa kulia, alipoulizwa kuhusu gomvi wake na babamkwe wake umesababishwa na nini, alieleza kuwa  ilisikika sauti kubwa ya kushtua na kutisha ikimuita ‘Sarah njooo kwa jian la yesu”jambo lililimfanya babamkwe kumpiga na mpini wa jembe mkwe wake na kumfukuzia mbali. Jambo la kushangaza, binti alizidi kueleza kuwa  mipini ya jembe waliokuwa wanatumia kulimia huko msukuleni ni mikono ya wanadamu!! Hakika hakuna lililositirika ambalo halitajulikana. Sarah amefunguliwa na yuko huru kwa jina la yesu.

 USHUHUDA WA RATIFA SIRAJI
    HAKUNA jambo gumu la kumshinda MUNGU! Hata hili ni jepesi machoni pa bwana! RATIFA SIRAJI ni binti aliyekuwa wakala wa shetani  aliyechukuliwa kwa njia ya kichawi na kuwekwa chini ya mto Wami huku kazi yake ikiwa ni kusababisha ajali na kuchukua matumbo ya uzazi ya wanawake kwa njia za kichawi na baada ya hapo alidai wanawake huenda hospitali na kupimwa na kukutwa na matatizo ya kizazi na huishia kukatwa. Jambo la kushangaza binti huyu aliyeonekana mwenye umri mdogo aliezeza kuwa hata alipokuwa anarudishwa alikuwa anatoka matekani alikuwa ametumwa  kusababisha ajari ya gari la MASAMA-SERENGETI ili kuchukuwa vizazi vya akina mama watakao kuwa katika gari hiyo. 
.
Ratifa akikana kumfahamu rafiki yake ambaye wanafahamiana vizuri
Jambo la kushangaza   mara baada ya kurudishwa binti  alikuwa hamtambui mtu yeyote hata yule aliyekuwa naishi nae nyumbani kwao. Hakika yake tunaokolewa kwa neema, hata leo neema ya Mungu ya ukombozi kwa walioibiwa na kutekwa imemfikia mtoto huyu na kumuokoa. Kwa kushuhudia zaidi alieleza kuwa mara baad ya kusikia sauti yenye mungurumo ikimuita “NJOOO” bibi aliyefahamika kwa jina la AMINA ambaye anadaiwa kumchukua na kumuweka mateka aliamua kumtupa katiaka viwanja vya mashujaa. Binti alipata kuombewa na mchungaji kiongozi JOSEPHAT GWAJIMA mpaka ufahamu wake na kumbukumbu zikarejea akawatambua ndugu zake. Yesu ni Yule yule jana leo na hata milele.
Ratifa Siraji akiwa amepona na ameshammpokea Yesu, na kuwekwa huru kutoka katika vifugo vya kumtumikia shetani

Binti aliyekuwa amechukuliwa msukule na hapa pichani akiwa amerudi anamshkuru Bwana Yesu na  Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima.
HAPPY MANDALI

       HAPPY MANDALI ni  binti mwenye umri wa miaka 16, anaishi mjini Moshi, amepata kurudishwa toka msukuleni alikochukuliwa na rafiki wa mama yake, ambaye ni mfanya kazi mwenzake.
  Dada huyu anayeitwa happy alionekana mwenye huzuni kubwa iliyoambatana na kilio kikubwa! Jambolilimfanya kuendelea kumsihi mchungaji kiongozi Josephat Gwajima aendelee kumuita mama yake maana binti alidai kuwa amemuacha pia mama yake kule msukuleni ARUSHA. Binti alizidi kusisitiza kuomba mama yake aitwe kwa kuwa aliona mateso na taabu alizokuwa akizipata kule msukuleni.Maandiko lazima yatimie kuwa mwana wa adamu alikuja kutafuta kila kilichopotea hata leo walokuwa wamepote wanaonekana na kurudishwa kwa jina la YESU



USHUHUDA WA AISHA MOHAMED
ASHA MOHAMED ana umri wa miaka 19, amekuwa mjumbe wa shetani kwa kufanyishwa mambo mazito na ya kutisha tangu akiwa na umri wa miaka 8. Asha ameweza kueleza mambo aliyoyatenda japo ilikuwa ni ngumu sana kuongea kutokan na ukweli kwamba alikuwa anasikia uchungu sana kwa kuwa alijiona kuwa mambo hayo yote hakuna wa kumsamehe makosa yake na watu wange mtenga.Lakini Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima alimshauri kuwa Mungu anasamehe kila dhambi hata iwe na ukubwa kiasi gani, cha msingi ni ukiri kuwa umekosa ujinyenyekeshe mbele zake na usiyarudie tena.


Hatimaye Asha akaelewa na akaanza kueleza, kuwa wakati anasoma darasa la nane nchini Kenya, ulikuwa usiku wa manane walimjia kundi la watu wengi wakamzunguka alikokuwa amelala na kumwambia unahitajika kijijini kwenu. Kulipokucha mchana wa saa sita, walikuja wasichana 3, wakiwa uchi walimfunika machoni na gafla alijikuta yuko kijijini kwao katikati ya kundi la wachawi wa kijijini.



Baada ya kuchukuliwa, alianza kufunzwa jinsi ya kuroga, na mwalimu wake alimtaja kwa jina la Hamis. Asha liendelea kupewa kazi na majukumu  kama kubadilishwa maumbile na kuwa mwanaume nakuanza kuwaingiia wanawake usiku jambo lililokuwa likisababisha wanawake kuvunja ndoa zao. Na wakati mwingine alikuwa akiwaingilia wanawake kwa kugeuzwa maumbile alikuwa nasababisha saratani na kupooza. Jambo la kusikitisha sana Asha amekuwa mateka kwa muda wa miaka 11 huku chakula chake kikiwa ni kunywa maji ya chooni!

 Aisha akionesha mkono ambao kulikuwa na kidole cha kichawi ambacho kilikuwa kimeoteshwa kichawi kwa ajili ya kuwanyonya watu damu na kuwasababishia kupooza.


Asha aliendelea kueleza kuwa alikuwa anatumia kucha yake ndogo ya mwisho kuchoma watu shingoni na kunyonya damu mpaka  kumsababishia mauti. Aliendelea kulia sana akidai kuwa amemnyonya damu mdogo wake mwenye umri wa miaka miwili, na pia alisema magonjwa kama ya saratani, na kupooza ni magonjwa ambayo yeye alikuwa anatumwa awasabishiye watu wengi sana.




Aisha Mohamed akiwa anakiri kuwa amechoshwa sana na kazi za ushirikina, akasema anataka kummpokea Yesu, akamkiri Yesu Kristo kuwa Bwana na Muokozi wa maisha yake, na akaokoka.

Saturday, October 26, 2013

MTOTO WA MCHUNGAJI APONYWA KATIKA MKUTANO WA MCH. JOSEPHAT GWAJIMA - MOSHI.




Mchungaji Kapange, wa mjini moshi baada ya kutoka kwenye mkutano wa Mch.Kiongozi josephat Gwajima, na kuona jinsi watu maelfu kwa maelfu wanavyo rudishwa kutoka katika vifungo vya shetani kwa kuitwa njoo na kuitiwa kwa Jina la Yesu, aliona ni vyema akajaribu kuyatumia maarifa na mamlaka hayo nyumbani kwake kwa mwane wa kike aitwaye Herrith
.



Baada ya kumuita kwa muda kidogo tu, mtoto akashtuka kwa nguvu sana, na kuanza kumuhoji baba yake ambaye ndiye mchungaji aliyeyabeba maarifa hayo kutoka mkutanoni, na kumuuliza hapa ni wapi baba?, mbona mimi skua hapa...

ndipo Mchungaji kapange alipo amua kukoleza moto na kumrudisha mtoto wake vizuri na baada ya hapo akamuweka ufahamu wake sawa kwa kumuombea tena kwa Jina la Yesu,na kumuwekea ulinzi wa Damu ya Yesu, ndipo mtoto alipoanza kutoa ushuhuda wake kuwa alikuwa anaishi kuzimu, na dude linaloaminika kuwa ni shetani aitwaye, mkuu wa kafara pia baba yake akamuuliza kwa nini kila siku nilipokuwa nakuuliza kama unashida yoyote hukuwa unasema? , mtoto akajibu kuwa alikuwa amefungwa na haoni na wala hawezi kusema, na alipohojiwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima wakati akitoa ushuhuda wake mbele ya mkutano alidai kuwa alikuwa amechukuliwa na mtu anayeitwa KANUMBA...na uwanja mzima ukalipuka kwa mshangao na haikuweza kujulikana kwa haraka ni kanumba yupi aliyemchukua, ama mwigizaji au ni jina la mchawi wa mtaani kwao.

"Na ndio maana kama kuna wakuchukia Duniani, ambaye anatakiwa abezwe na watu wote ni mchawi anaye "m-host"  shetani - -Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima akiwa katika picha ya pamoja, na baadhi ya waliofika mkutanoni na kupokea miujiza yao na kuwekwa huru kutoka kwenye vifungo mbalimbali vya shetani hasa hasa ilikuwa ni siku ya kuzivunja laana za familia, na kuwaweka huru ambao walikuwa wako msukuleni. Nyuma ya mchungaji kiongozi ni Mchungaji Mwandamizi Mkuu (SRP) Grace Gwajima na aliyevalia kofia ya kiaskari ni Mchungaji Mwandamizi (RP) Maxmillian Machumu.

Friday, October 25, 2013

ALIYEKUWA AMEPOTEA KWA MIAKA MINNE APATIKANA BAADA YA MAOMBEZI MKUTANO WA Mch. Josephat Gwajima - Moshi..


   Mama mmoja mkazi wa Moshi, apokea muujiza wake wa kumpata mwanae aliyefahamika kwa jina la YONA HONEST aliyekuwa amepotea katika mazingira ya kutatanisha kwa kipindi cha miaka 4 iliyopita. Mama huyu mara baada wa kuhudhuria mkutano kwa mara ya kwanza, aliamua kuchukua hatua ya kuandika
 
Jina la mwanae aliyekuwa amepotea. Mshangao ulitokea pale kijana huyu alipokuwa anaelezea kuwa alikuwa amewekwa mateka huko mkoani Tanga, huku mama Yona anashuhudia kuwa  baada ya kufika kwenye mkutano Yona amepatika Mkoani Dodoma na kuweka kwenye box. Mama YONA akiwa katika hali ya furaha huku akimtazama kijana wake alimshukuru sana Mungu kwa kumrudisha mtoto wake, aliyedai kupotelea Tanga huku akifanyishwa kazi ya kukamua ng’ombe aa watu maziwa kwa kipindi chote hicho. 
BINTI MARY KISIMBO


Binti huyu anaitwa Mary Kisimbo anatoa ushuhuda wake kuwa alikuwa amewekwa makaburini, na bibi mmoja ambaye hamfahamu vizuri,lakini ni mweusi sana.Baada ya maombezi ya Mch. kiongozi Josephat Gwajima,  Anadai alianza kuisikia sauti inamuita njoo kwa jina la Yesu na akashtukia yuko uwanja wa mashujaa. Binti huyu alimshukuru Bwana Yesu kwa kumuweka huru kutoka kwenye kifungo hicho cha shetani na akaahaidi kumkabidhi Mungu maisha yake na kumtumikia.




   Baada ya kuvunja laana za familia, JANETH SHIRIMA aliyechukuliwa katika mazingira ya kichawi na kuishi Mombasa, aliachiwa huru na waliomchukua wakidai kuwa hafai, !! 
Mwana mama huyu alisema kuwa baada ya mchungaji kuomba juu ya mji wa moshi huku akitamka “moshi na mitaa yake, moshi na laana zake, moshi na watu wake “njooooo” sauti hii ilisikika katika sahemu alikokuwa binti  huyu ameshikiliwa na wakamtupa wakmuachia . JANETH anashuhudia kuwa jumla ya mabinti 10,000 wenye umri mdogo  aliwachukua na kuwafanya machangudoa (wakiuza miili yao). Janeth alisisitiza kwa sauti ya hasira kuwa wachawi wa pigweeee kwa JINA LA YESU.
 AMINA SELEMANI

Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akimuombea binti huyu anayeitwa Amina Selemani, ambaye alikuwa amefichwa kishirikina kwenye mashamba huko mkoani Tanga, likuwa akilishwa nyama za watu, na kulazimishwa kushiriki mambo ya kichawi baada ya maombezi ya Mch.Gwajima aliskia sauti inamuita njoo kwa jina la Yesu alikuja na usafiri wa ungo ambao kuna watu walikuwa wamembeba na kummbwaga.
 GLORY SHAYO
Binti huyu anaitwa Glory Shayo, anaelezea kisa chake, kuwa, siku moja alikuwa shule ghafla akazimia kwenye mida ya saa saba, lakini baada ya muda mchache akazinduka, half saa nane tena akazimia , akaamka yuko hopitali ya St.Joseph lakini akaambiwa hana ugojwa ,ila ndio ukawa mwanzo wa kuanza kushambuliwa mara kwa mara na magonjwa mbalimbali ambayo hakuna hospitali inayompa maelezo mazuri ni ugonjwa gani hasa unaomsumbua, baada ya kufika kwenye mkutano, na kufuata maombezi ya mchungaji josephat Gwajim, kuwa kila mtu uwanjani asemae anaomba kumuona yule mtu muovu anaye lta uadui katika masiha yake ndio ghafla akashtukia chini na akmuona aliyekuwa akimtesa, kumbe ni mtu wake wa karibu, aliyekuwa amedhamiria kumfanya ashindwe kabisa kusoma shuke, ambaye aliweza kumtaj kwa jina moja tu kuwa ni Halima,


Mchungaji Kiongozi wa kanisa la ufufuo na uzima akistaajabishwa na habari za Binti huyu ambaye, analezea mbele ya watu kuwa alikuwa nchini Congo alikopelekwa na bibi yake,ambako alikuwa amechukuliwa kiuchawi na kuwa msukule katika nchi hiyo ya Congo na kazi yake kubwa ilikuwa ni kuuwa watu kwa njia za uchawi,ila baada ya maombezi ya Mch. Kiongozi Josephat Gwajima alisikia sauti inamwuta njoo na ghafla akaletwa na aliyemchukua kwa kutumia usafiri wa kichwa cha mtu.
 GUDIRA JOSEPH MUSHI


  Moshi yote kwa YESU! Hata aliyekuwa mtoni sauti ya njoo imemfikia.GUDIRA JOSEPH MUSHI, ameisikia sauti ya njoo leo akiwa mto Rau ulioko mjini Moshi, yaliyokuwa makao yake. Binti huyu leo amerudishwa toka msukuleni nakueleza alivyo kuwa akisababisha ajari na kusimamisha magari katika eneol a mto RAU.Gudira alionekana kupigwa na butwaa huku akishangaa mazingira ya kusanyiko la watu wengi,wakati anadai kuwa amezoa kuishi majini, huku viumbe vya majini vikiwa ndo marafiki zake. Asifiwe Mungu wa wote wenye mwili aliye mtoa katika makao ya kuzimu.


MCHUNGAJI KAPANGE

    Mchungaji Kapange, wa mjini moshi baada ya kutoka kwenye mkutano wa Mch.Kiongozi josephat Gwajima, na kuona jinsi watu maelfu kwa maelfu wanavyo rudishwa kutoka katika vifungo vya shetani kwa kuitwa njoo na kuitiwa kwa Jina la Yesu, aliona ni vyema akajaribu kuyatumia maarifa na mamlaka hayo nyumbani kwake kwa mwane wa kike aitwaye Herrith.

Baada ya kumuita kwa muda kidogo tu, mtoto akashtuka kwa nguvu sana, na kuanza kumuhoji baba yake ambaye ndiye mchungaji aliyeyabeba maarifa hayo kutoka mkutanoni, na kumuuliza hapa ni wapi baba?, mbona mimi skua hapa...
ndipo Mchungaji kapange alipo amua kukoleza moto na kumrudisha mtoto wake vizuri na baada ya hapo akamuweka ufahamu wake sawa kwa kumuombea tena kwa Jina la Yesu,na kumuwekea ulinzi wa Damu ya Yesu, ndipo mtoto alipoanza kutoa ushuhuda wake kuwa alikuwa anaishi kuzimu, na dude linaloaminika kuwa ni shetani aitwaye, mkuu wa kafara pia baba yake akamuuliza kwa nini kila siku nilipokuwa nakuuliza kama unashida yoyote hukuwa unasema? , mtoto akajibu kuwa alikuwa amefungwa na haoni na wala hawezi kusema, na alipohojiwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima wakati akitoa ushuhuda wake mbele ya mkutano alidai kuwa alikuwa amechukuliwa na mtu anayeitwa KANUMBA...na uwanja mzima ukalipuka kwa mshangao

"Na ndio maana kama kuna wakuchukia Duniani, ambaye anatakiwa abezwe na watu wote ni mchawi anaye "m-host"  shetani - -Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima

Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima akiwa katika picha ya pamoja, na baadhi ya waliofika mkutanoni na kupokea miujiza yao na kuwekwa huru kutoka kwenye vifungo mbalimbali vya shetani hasa hasa ilikuwa ni siku ya kuzivunja laana za familia, na kuwaweka huru ambao walikuwa wako msukuleni. Nyuma ya mchungaji kiongozi ni Mchungaji Mwandamizi Mkuu (SRP) Grace Gwajima na aliyevalia kofia ya kiaskari ni Mchungaji Mwandamizi (RP) Maxmillian Machumu.