Tuesday, September 9, 2014

THIS IS MY STORY: Ushuhuda wa Kichaa cha Naomi


THIS IS MY STORY   -  JUMAPILI  07.09.2014

Mwalimu Malinga na mke wake, wameokoka muda mrefu sana na ni wakazi wa Bigwa Morogoro. Kabla ya tukio hili, Mzee Malinga alikuwa Kiongozi (Mzee wa kanisa) katika Kanisa la TAG - Moria (lililopo Mtaa wa Kola B - Morogoro).


Mzee Malinga (katikati), mkewe (kushoto) na Baba
(SNP Dr. Godson), wakati familia hii  ikishuhudia
matendo makuu ya Mungu kwa mtoto wao Naomi.
Familia hii wana mtoto anayeitwa Naomi, ambaye alifaulu vizuri form 4, na
tarehe 27 March 2014 ilikuwa birthday yake. Hata hivyo, Jioni ya hiyo siku ya tarehe 27 March mwanae alianza kuona watu ambao walikuwa wanamfuata sebuleni ingawa baba yake alikuwa hawaoni. 


Katika wale watu aliokuwa anawaona miongoni mwao ni  majirani za familia hii, na ambao miongoni mwao watoto wao hawakuwa wamefaulu kama Naomi. 


Usiku ule Naomi (mwanae) alikuwa anakimbia kimbia ovyo, na kumgongea mlango baba yake akisumbuliwa na wale wachawi. Maajabu Naomi alikuwa na macho ya kuona watu ambao wasioonekana kwa baba yake waliokuwa wanamvizia. Ndiposa Baba yake aliwaza pengine ni malaria imepanda kichwani kwa mwanane. 


Kuna wakati baadae baba alitaka kumsaidia mwanae, lakini looh, Naomi akamwambia baba yake kuwa amechelewa na huyo  mtu aliyekuwa anamfuata akimvizia kutaka kumchinja na kisu na keshaondoka zake.


Mama mzazi wa Naomi alikuwa ameenda Moshi kipindi hiki cha kuanza kwa hili  tatizo. Baba yake Naomi alimpeleka kwa Mchungaji wa TAG ambapo anaabudu, na akafanyiwa maombi na kuazimia kumuacha kwenye hii nyumba ya mchungaji. Hata hivyo mwanane kuanzia siku ile alikuwa halali kabisa usingizi wowote.


Siku moja Naomi alitoroka na alipopatikana alipelekwa hospitalini, ingawa alikutwa hana tatizo kubwa la malaria, kwani hakuwa na vimelea vya malaria vyenye kuhitaji matibabu. 



Siku iliyofuata alipatiwa tiba nyingine ya 'quinine' na kila mara akawa anaongezewa dozi. Madakatari walikiri aina hii  ya malaria haijawahi  kufahamika au kuwepo kwenye taaluma zao. Madaktari  walipendekeza pengine aanzishiwe dozi ya wenye vichaa. 


Dozi ilianza lakini pia wazazi na madkatari wakapendekeza kuwaona watumishi wa Mungu. Muhimbili ikawa sehemu ya mwisho, na ambapo madaktari walishauri kama wazazi wanataka kwenda kwa waganga wa kienyeji sawa, au makanisani kuombewa sawa, wafanye hivyo. 


Wazazi walimpeleka Majumba Sita  Dar es Salaam akaombewa penye kanisa la TAG, na baada ya maombi, Naomi akawa ametulia na kulala. Walimuacha mwanae mahali pale akiombewa, na huku ile hali inamrudia kila baada ya  siku. 


Muda wa mwanae kwenda shuleni  ukawadia,  na wazazi wakaenda kumchukua kutoka huko Dar es Salaam. Hata hivyo fujo ziliendelea  kuwa kubwa zaidi, na Naomi alikuwa akitaja majina ya watu wakubwa serikalini, na hata wasanii kama akina Kanumba n.k. alipotajiwa kwenda shule,  ndipo kabisa aligoma katakata  na kusema hana mpango wa kwenda shuleni tena.


Wapo ndugu waliomshauri ampeleke Moshi kwa sababu kuna sehemu ya maombi mazito. Mzee Malinga kwa kujali alifunga safari  kwenda Moshi na Naomi. Ilibidi amfunge miguu mwanae ili asimtoroke. Njiani alipata shida sana kumepleka, kwani alikuwa anakataa kufuatana na baba yake na hata kunyanyuka  kwenye kiti cha basi  na kuanza kucheza nyimbo za TV ya lile basi mbele ya abiria wote.  


Mbaya zaidi,  Naomi akiwa njiani alikuwa anasema baba yake  anataka kumtoa kafara, jambo ambalo lilifanya abiria waingilie kati na kujua kulikoni? Walipofika Moshi,  mzee huyu alikodi Guest House yenye double beds ili kuhakkikisha kuwa mwanae hatatoroka, lakini  mwanane akagoma kulala akipiga makelele kwamba baba yake amefanya hivyo ili apate nafasi ya kumbaka. Baba huyu alijisikia vibaya sana na aibu ikawa inampata. Palepale  Baba yake  alipewa wazo la kutafuta hosteli ya masista pale Moshi na
ambapo  mwanane alikubali kulala pale hosteli.


Kesho yake alimpeleka mwanae  kwa 'Yule  Mtu wa Maombi'. Mzee Malinga anakiri kuwa toka amekulia wokovu hakuwahi kukutana na aina hii ya maombi. Kwa nini? Anasema ni aina ya  maombi ambayo mwanae aliambiwa aizunguke madhabahu,  na kisha kunyweshwaa maji ambayo hakufahamu yana kitu gani. Hata hivyo maombi yale hayakumsaidia mwanae.


Alirudi Morogoro, ikabidi wampeleke upya Naomi Hospitalini, na ambapo madkatari walishauriana kumuanzishia huyu mtoto dozi ya kutuliza watu wenye kichaa.  Pale hospitalini hata hivyo, alikuwepo Dr. Loice wa Hospitali ya Saba saba (Majeshi Majeshi) ambaye aliwashauri wazazi hawa wampeleke Naomi Kanisani Ufufuo na Uzima Morogoro,  kwani alibaini kuwa tatizo kama hili tiba yake siyo ya Hospitalini tena. Hata hivyo, wazazi walikuwa na taarifa hasi dhidi ya Kanisa hili. Walijishauri sana juu ya  wazo hilo, wakisema endapo makanisa yote waliyokwenda shida ya Naomi haikutatuliwa,  je, Kanisa la Ufufuo na Uzima watawezaje? Hata hivyo  walitii na kesho yake wakafika kanisani ambapo walipokelewa vizuri na maombi kwa Naomi yakaanza rasmi. Kuanzia siku ile, Naomi alianza kufunguliwa na kuanza kurudiwa na ufahamu wake. haikuchukua muda mrefu, wazazi wakiwa wanamleta Naomi kwenye Mkesha na Ibada za katikati ya wiki, Naomi akawa mzima kabisa.



Baba na Mamawa Naomi Malinga wakitoa sadaka ya
Shukrani na Dictionary ya Biblia kumshukuru Mungu
aliyemponya Naomi kutoka kwenye Maradhi /
Ukichaa wa kutengenezwa  07/09/2014.
Wazazi wa Nomi kwa pamoja  wanakiri kuwa Naomi amepona kabisa na sasa amejiunga na shule ya Sekondari Mpanda na hata walimu wake wanakiri kuwa Naomi ni mzima kabisa. Baba na mama wa Naomi wameamua mchana kweupe  kujiunga na Kanisa la Ufufuo na Uzima Morogoro. Wanahuzunishwa sana na tuhuma zilizokuwa zinafanywa dhidi ya Kanisa hili kulichafua kuwa ni mojawapo ya 'frremasno'. Wazazi hawa kwa pamoja  wameamua  kuwa  wapo tayari kumtumikia Mungu wa Ufufuo na Uzima kwa matendo ambayo wameshuhudia Mungu huyu akifanya, na zaidi sana kwa kumponya Naomi.

Tuesday, April 8, 2014

UJAUZITO WA MIEZI KUMI NA MBILI NA KUZAA MTOTO WA AJABU - PATA USHUHUDA WAKE

===================THIS IS MY STORY=============
JUMAPILI 06 April, 2014...... (Ufufuo na Uzima - Morogoro)
USHUHUDA WA LEO: THIS IS MY STORY, BY CESILIA (Part One)
Utangulizi: Cesilia Alilkuwa ameolewa Tanga na mwanaume ambaye alikuwa mganga wa kienyeji, ila hakuwahi kumweleza ukweli kuwa ni mganga. Alipata ujauzito uliodumu kwa miezi 12 na kisha akaamua kwenda kwa mganga wa kienyeji kuaguliwa. Mganga akamwambia anatakiwa apatiwe dawa ya kuishusha nyota yake. Alimletea dawa ambayo ni mavi ya tembo, ambayo alitakiwa akoroge hiyo dawa nyakati za saa nane usiku ainywe. Alitakiwa atumie sumaku kuishusha hiyo dawa kuanzia kifuani hadi tumboni ili hapo kesho yake aweze kujifungua. Hata hivyo ilipofika kesho yake hakujifungua.

Wengine walimwambia aende kwa bibi yake kijijini. Bibi huyo alimpeleka kwa mkunga. Mkunga alimwambia inaelekea hiyo mimba ni kubwa sana, ila anachotakiwa ni kuwa akipata tu uchungu aende hospitali. Cesilia aligoma kwenda hospitali akisema “kama ni kufa na nife tu”, haya aliyasema akiwa nyumbani kwake.
Siku ya siku ililazimu kwenda hospitalini, ambapo walimwambia inaelekea ana mimba ya Watoto wanne. Hata hivyo hospitalini pale manesi walikuwa wananong’onezana wao kwa wao kwamba huyu mgonjwa ni wa kufa, na hakuna uwezekano wa kupona. Pale hospitalini madktari waliitana na kumwambia asaini hati ya kufanyiwa operesheni. Wakati wa kufanyiwa ile operesheni, ghafla alikosa fahamu, kisha akajikuta yupo mahali ambapo wamejaa Waarabu, na walikuwa wanachezea midoli. Waarabu hawa Walikuwa wakimlazimisha apokee hiyo midoli, lakini akakataa. Baada ya kuzinduka usingizini, alimkuta mdogo wake pembeni mwa kitanda. Alimuuliza dada yake kipi kinaendelea akaambiwa, tayari ameshafanyiwa operesheni na mtoto wako yupo kwa manesi. Aliomba kupatiwa mtoto amuone, lakini alipoletewa kumuona, alishangaa kumuona mtoto wake kuwa na kichwa kikubwa sana. Mtoto huyu alikuwa mlemavu kiasi kwamba hawezi kugeuza kichwa chake.

Ndani ya Mwezi mmoja wa kuishi kwa yule mtoto tayari alikuwa na uwezo wa kuongea maneno kama ‘mama hamna, baba, babu’….. Huyu mtoto nyakati nyingine alikuwa na vituko kiasi kwamba majirani wa kiislamu walikuwa wanamtia moyo mama huyu, eti katika dini yao Watoto kama hao wapo, na ni maalumu kwa kutoa shuhuda. Pamoja na kwamba mtoto huyu alikuwa hawezi kujiegeuza, lakini nyakati za usiku mama yake alikuwa akiamka anamkuta huyu mtoto akiwa kwenye titi ananyonya, na akawa anajiuliza ni nani anayemsaidia kumweka mtoto kwenye titi bila kupata majibu.......!!!!

Siku moja alitokewa na majini matano. Hawa walikuwa wamevaa baibui, wakamtishia wakisema, “wewe ni wifi yetu, uliolewa na kaka yetu, na sasa hutaki kumleaa huyu mtoto. Kuna siku tutakuja kumchukua huyu mtoto, tutakupa pesa, na ukifanya mchezo tutaondoka na wewe pia ili ukamlee huyu mtoto”. Walimpa Tarehe na muda wa kuja kumchukua huyu mtoto. Siku tatu kabla ya Tarehe majini waliyosema ni ya kumchukua mtoto huyu, alipata wazo la kuchangisha michango akitumia picha ya yule mtoto ili mtoto akapatiwe matibabu ya kichwa chake. Waliomshauri walimwambia apite kwenye maduka ya WAARABU na WAHINDI kwani ni wazuri sana kwenye kuchangia mambo kama haya, naye akafanya hivyo.

Mama alivyorudi aliambiwa mwanao amekunywa maziwa kikombe lakini papo hapo akatapika puani mitihili ya maji maji. Mama alimuitaa mwanae kwa jina lake la Robert, naye akamuitikia mama yake, huku akimpangusa machozi mama yake. Hata hivyo alikufa baadae kidogo na kupelekwa kijijini kwa mazishi, wakitumia pesa ile ya michango ya jana yake, sawasawa na lile neno aliloambiwa na yale majini kuwa watampatia pesa. Walifanya mazishi ya haraka haraka nyakati za usiku kwani waliokuja pale walishauri maiti asikae muda mrefu kwani alikuwa anaumuka na kuongezeka umbile lake. Bwana wake alikasirika sana mwanae huyu kuzikwa mahali nje ya Njombe kwani alikuwa ni mzaliwa wake wa kwanza.

Bwana wake alianza kujidhihirisha kuwa ni mganga kweli kweli. Aliamua kumpeleka mke wake huyu Ukerewe ili apewe cheo kikuu cha kufanya uganga. Mashekhe walimlazimisha mama huyu abadili dini lakini akagoma. Baadaye walifanya dawa zao ambazo zilileta kizazaa kwa mtoto mwingine wa mama huyu aliyemzaa na mume mwingine kabla ya kuanza mahusiano na bwana huyu mganga. Hata hivyo bwana huyu alimpa dawa/mitishamba mtoto huyu wa kambo na akapona.

Baadaye bwana huyu alihamia Kiteto, kijiji cha Dosidosi ambako alimuita mke wake wakae pamoja ili amsaidie kwenye kazi ya kuvuta wateja. Huyu mama alimfuata, na kisha akawa na kazi ya kuandika maneno yote ya kiaguzi / kiganga pindi wateja wanapokuja kufanyiwa uganga. Miongoni mwa dawa za mganga huyu ni unyayo wa bata na kiini cha yai la bata. Kwa hiyo maisha ya kula kuku-nyama yakamfurahisha sana huyu mama, na kujiona yupo salama. Baadae siku moja baada ya kufanyiwa uganga usiku, ndipo tatizo la kutokwa damu mfululizo likamuanza huyu mama.

Alipoona hali yake ya kutokwa na damu inaendelea kumsumbua, alienda Hospitalini ambapo alipata vipimo vyote, na kukutwa na magonjwa mengi tu kama vile typhoid, Ukimwi, malaria kali, ukosefu wa damu n.k. Siku ya 69 baada ya damu mfululizo kuendelea kumtoka huyu mama, aliletwa hapa kanisani (UFUFUO NA UZIMA – MOROGORO) kuombewa, baaada ya kupewa ushauri huu na baba mdogo wake anayeitwa Amani. Baada ya Maombi, damu yake ilifunga papo hapo. Bwana wake alipiga simu siku hiyo hiyo akilaumu kwa nini amepelekwa kanisani badala ya kupelekwa kwa mashekhe wawili kufanyiwa tiba mbadala. Usiku wake huyu mama aliota ndoto kuwa amekutanishwa na babu yake ambaye ni marehemu. Bwana wake akawa anampigia simu mkewe huyu kusema, amemvurugia mambo yake. Mongoni mwa shutuma nyingine ni kuwa, balaa zilikuwa zinaikumba sana familia ya huyu bwana, ikiwemo ajali za pikipiki na moto kwa ndugu zake. Nyakati nyingine alimpigia simu mkewe kumwambia eti Maombi ya Wakristo ni sawa na uchawi.
==USHUHUDA HUU SEHEMU YA PILI UTAENDELEA WIKI IJAYO==

==Na Mwandishi Wetu==
== Information Ministry (Ufufuo Na Uzima - Morogoro)==
PICHANI: Cesilia akielezeea ushuhuda wake (part one) katika Nyumba ya Ufufuo na Uzima - Morogoro Jumapili 06 April 2014. Kushoto kwake ni AP Steven Nampunju na Kulia ni SNP (Baba) Godson Issa Zacharia wa Ufufuo na Uzima - Morogoro

Wednesday, March 19, 2014

ANASWA UFUFUO NA UZIMA - ARUSHA AKIWA ANAFANYA UCHAWI


Katika hali isiyo ya kawaida mtu huyu ajulikanaye kwa jina la Shabani Hamis amenaswa akiwa anafanya uchawi katika kanisa la Ufufuo na Uzima Arusha.



Matukio ya kunaswa wachawi yamekuwa mengi kanisani hapo kutokana na uweza wa Mungu unaojidhihirisha kupitia Mchungaji Kiongozi wa kanisa hilo, Frank Andrew.

Pamoja, na kukutwa bila nguo mtu huyo aliyekuwa amebeba vifaa ambavyo kwa mujibu wa maelezo yake, huvitumia kuwanga na kupaa. Tukio hilo la aina yake limetokea Usiku wa saa sita, wakati mkesha wa maombi ukiendelea kanisani hapo.

Baada ya maombi makali ya kuharibu uchawi katika anga la Arusha, ikafuatiwa na tukio hilo. Mungu ni mkuuu maana hapana uchawi wala Uganga juu ya watu wa Mungu.