Tuesday, December 24, 2013

APONYWA MAUMIVU YA TUMBO BAADA YA MAOMBEZI UFUFUO NA UZIMA - MOROGORO

 Binti anayeitwa Amina Salum ambaye hapo awali kabla ya kuokoka alikuwa muislamu, alikuja katika mkutano wa Ufufuo na Uzima akisumbuliwa na magonjwa mbalimbali ambayo yalikuwa yakimsumbua.

Akieelezea tatizo lake, Amina alisema kuwa alikuwa na tattio la tumbo ambalo alikuwa akisikia kuwa tumbo linachomachoma ndani kiasi cha kushindwa kula. tatizo ambalo lilimnya adhohofu mwili siku hai siku.

Wakati Mhungaji Gwajima akipita katikati ya makutano alimkuta amekaa na mapepo walipomuona Mchungaji wakalipuka ndani yake ambapo yaliamriwa yatoke ; na baada ya kumtoka Amina akawa huru kabisa na akapokea muujiza wake. na tokea hapo, maumivu yote ya tumbo yaliyomsumbua miaka mingi yakaisha.
mUNGU KWETU SISI NI MUNGU WA KUOKOA NA NJIA ZA KUTOKA MAUTII ZINA YEYE.
Mchungaji Gwajima akiwa amemshika Amina baada ya maombezi.

Wednesday, December 18, 2013

MCHAWI ANASWA KATIKA MKUTANO WA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO


Ikiwa ni siku ya tatu ya mkutano wa ufufuo na uzima unaoendelea katika viwanja vya vya shule ya sekondari ya morogoro mchawi mmoja aliyejulikana kwa jina la Fatuma amekamatwa katika mkutano huo akiwa yuko katika shughuli zake za kila siku za kichawi.

Dada huyo aliyekamatwa na Nguvu za Mungu alielezea akasema alikuwa na wenzake ambao walitumwa na bosi wao ambaye ni mchawi na mganga wa kienyeji maarufu kutoka mjini Bagamoyo wilaya ya pwani kuja katika mji wa Morogoro kuchukua miili ya watu waliokufa katika nyumba za kuhifadhia maiti za hospitali(mochuari) kwa ajili ya kitoweo.

Akizungumza alisema yeye na wenzake walipoteana walipofika karibu na hospitali ya rufaa ya mji wa Morogoro ambapo ni eneo la jirani na sehemu mkutano unapofanyika, alipofika maeneo hayo alisikia nguvu inamvuta kwa nguvu na kumpeleka asipotaka yeye ndipo alipojikuta ametua katika viwanja shule ya sekondari ya Morogoro ambapo ndipo mkutano unapofanyika
Dada huyo aliyeonekana kuwa na wasi wasi alisema tulikuja mimi na wenzangu kwa usafiri wa njia ya fisi lakini tulipokaribia hospitali sijui nini kimetokea na mimi nikasikia nguvu zinanivuta nikajikuta niko mahali hapa

ALIANZAJE UCHAWI

Akielezea jinsi alivyoanza uchawi alisema miaka kumi na tano iliyopita alikua anaumwa ndipo alipoamua kuondoka kwao Babati(Manyara) kwenda kutibiwa mkoani Pwani kwa mganga aliyejulikana kwa jina la Idi. Alipofika kwa mganga aliambiwa akachume pilini dawa Fulani na aitafune, alipofanya sawasawa na maelekezo ya yule mganga ndipo alipojiona anaanza kuingiwa na ukatili usiokuwa wa kawaida na akaanza kupata hamu ya kula wanadamu wenzake, kuanzia siku hiyo ndipo alipoanza kuagizwa na Idi kwa ajili ya kufanya shughuli za kichawi pamoja na wenzake.

NAMNA ALIVYOKUWA AKITENDA KAZI

Yeye na wenzake walikuwa wanawashughulikia hasa watu ambao waliokoka na baada ya hapo wakarudi nyuma, akieleza jinsi walivyokua wakiifanya kazi hiyo alisema mtu yeyote aliyewahi kuokoka na baada ya hapo kumuacha Yesu anakuwa na majini mawili wanaotumwa kukaa ndani yake, na wachawi hawa wanapomfuata mtu huyo wanaongea nayale mapepo na wanayaagiza yamnyonge mtu huyo na mtu huyo anakufa mara moja

Katika utendaji kazi wake yeye ndiye aliyekuwa kiongozi wa kikundi chake hicho walichokuwa wanatenda shughuli hizo za kichawi.Alisema mimi niliwekwa kuwa kiongozi wa wenzangu kwasababu mimi nilikua nimefanikiwa kuwaua watu watatu waliokua wameokoka na kurudi nyuma. Kule kwenye uchawi mtu aliyefanikiwa kuwaua watu waliorudi nyuma ndie anakua na cheo kuliko wengine, mimi niliua watu ambao walikua hawajawahi kuokoka zaidi ya thelathini na waliokua wameokoka na kurudi nyuma watatu alisema dada huyo.

Akielezea alisema sisi tulikuwa na uwezo wa kuwaua watu kwa matukio tuliyokua tunayatengeneza, unaweza ukakuta mtu anatembea njiani alafu akawa kama ameumwa na nyoka lakini nyoka mwenyewe hamuoni, mtu huyo baada ya masaa machache atakufa na sababu itakuwa kwamba aliumwa na nyoka lakini sivyo tunakuwa ni sisi tumemtengenezea kifo ili tukamle nyama.

WATU ALIOWAHI KUWAUA

Alisema anakumbuka miaka mitano iliyopita alimuua mdogo wake aaliyekuwa anajulikana kwa jina la Udiyomboli, watu watatu ambao waliwahi kuokoka na kasha kurudi nyuma pamoja na wengine Zaidi ya thelathini aliowaangamiza kwa kutumia uchawi
Baada ya hapo dada huyo akiongea kwa huzuni aliomba msaada akasema, nimechoka kufanya uchawi siyapendi maisha haya na sitaki tena kurudi kule Bagamoyo.

Dada huyo tayari ameshaachana na mambo ya uchawi na amempokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yake.

Thursday, December 12, 2013

MWANAMKE ANAYESADIKIWA KUWA NI JINI AIBUKA NA KUTOWEKA MKUTANO WA MCH. GWAJIMA - JIJINI TANGA

Mkutano mkubwa wa Ufufuo na Uzima na mchungaji Josephat Gwajima umehitimishwa kwa tukio la aina yake lililosisimua watu waliohudhuria mkutano huo. Ni tukio la ajabu kutokea ikiwa ni siku moja tu mara baada ya mkutano wa Ufufuo na Uzima kuhamia katika jengo moja maarufu mkoani Tanga.

Mkutano wa Mchungaji Gwajima Tanga kabla ya kuhamia katika jengo jipya.
Pamoja na kufundisha kuhusu misukule, nyota, ndoto na kuhusu wafu; Mchungaji Gwajima alifundisha pia kuhusu majini na jinsi ya kuwashinda ambapo alisema wazi kuwa majini ni viumbe ambavyo ni vya rohoni na vinaweza kuvaa umbele lolote la binadamu au mnyama.

Akinukuu hay ya kitabu cha Shehe Falsihi wa zanzibar alisema "majini ni viumbe vya angani ambavyo havina viwiliwili hivyo huwezi kuviona kwa macho, lakini vinaweza kuvaa ima umbo la kifuu cha nazi au umbo lolote" alisoma haya hiyo akieleza kuwa uislamu na ukristo wote unataja viumbe hivi yaani majini.

Wakati somo likiendelea kukatokea jambo la ajabu ambalo kwa tafsiri ya rohoni ilikuwa ni uthibitisho wa kile ambacho Mchungaji Gwajima amekuwa akifundisha katika jiji hilo la Tanga.

Mchungaji Gwajima alipokuwa akizunguka katikati ya makutano ili kuwafungua wenye vifungo, zilisikika kelele za watu zikipiga kelel kuwa kuna mtu amevaa ushungi yupo kwenye kona ya bati. jambo ambalo lilivuta hisia za wengi. Kwani mwanamke huyo alionekana na watu wote akiwa kwenye bati la nyumba moja ya ghorofa pembeni mwa jengo la kuabudia.
Watu waliokuwepo wakiwa wanamshangaa muda mfupi kabla hajatoweka..  (Ghorofani amezungushiwa rangi)


Ni kweli kuwa kwa ghorofa lile hakuna ambaye angeweza kupanda, wala kukaa kule juu na ukizingatia ni mwanamke. Watu wakiwa wametaharuki na wengine kuliitia jina la Bwana ghafla mwanamke huyo akatoweka mbele ya macho ya watu wote na kuweka hofu miongoni mwa watu wote.

NI NINI TAFSIRI YAKE?
Akiongea jumapili hii kanisani, Mchungaji Gwajima amesema jambo hili ni udhihirisho wa kile alichokuwa anakisema; na ya kwamba yeye alimwona mwanamke huyo kabla watu hawajamuona na kwa kuwa Mungu amekuwa amekuwa akimwonyesha viumbe vingi vya rohoni akahisi kuwa watu hawajamuona. Alisema, "Mungu amekuwa akinionyesha viumbe vingi vya rohoni wakati nahubiri na mara nyingi huwa sitaki kuwatia hofu watu hivyo hukaa kimnya bila kuwambia "
Muda mfupi kabla ya Mwanamke huyu kutoweka Camera yetu ilimnasa

Kumbe ilikuwa ni uthibitisho wa Mungu kuwa viumbe hawa wapo na pia wanaweza kuvaa miili ya binadamu kama vile walaika walivyovaa mwili na kumwendea Ibrahimu na hawa wanavaa miili ili kutekeleza haja zao duniani. Majini ni halisi lakini kwa jina la Yesu wameshindwa kabisa na Tanga imekuja kwa Yesu.

Wakati huohuo eneo jipya la kuabudia la nyumba ya Ufufuo na Uzima - Tanga lipo katika hatua za mwisho za ukarabati ili lianze kutumika shuhudia pichani.



Tuesday, December 3, 2013

ALIYEIANGUSHA MELI YA MV SPICE HIGHLANDER AOKOLEWA KUTOKA KWENYE UTUMWA WA SHETANI KWA NGUVU ZA MUNGU KATIKA MKUTANO WA MCH.KIONGOZI JOSEPHAT GWAJIMA, JIJINI TANGA.

BINTI AITWAYE THERESIA AMBAYE ALIKUWA ANATUMIKISHWA NA SHETANI AELEZEA JINSI ALIVYOSHIRIKI KATIKA KUIZAMISHA MELI YA MV SPICE HIGHLANDER KWA NJIA ZA KISHETANI.
Theresia akiombewa na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima ili kumuweka huru kutoka katika kifungo cha kumtumikia shetani, pia alikuwa anamatatizo ya miguu na hapa anaombewa kwa jina la Yesu.

Theresia ni binti aishiye Jijini Tanga na Mama yake mzazi, na siku hii ambayo alifunguliwa kutoka kuzimu kwa shetani alikuwa amekuja kwenye Mkutano wa Injili uliokuwa umeandaliwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima Jijini Tanga na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima.
Theresia akiwa analia kwa uchungu punde tu..baada ya kutoka kufunguliwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akiwa anamuhakikishia kuwa kwa sasa tayari yuko salama na hatochukuliwa tena...kwa maana kwa Yesu ni salama Daima..

Na baada ya Mchungaji Josephat Gwajima kuanza kuwaombea maelfu ya watu ambao walikuwa mkutanoni wengi walifunguliwa, na waliokuwa katika vifungo vya shetani, na  misukuleni walifunguliwa na kurejeshwa katika hali zao za kawaida.


Mchungaji Kiongzoi Josephat Gwajima akiwa na Binti Theresia pamoja na Mama mzazi wa binti Theresia

Theresia akiwa tayari kuanza kuelezea habari nzima..



ALIFIKAJE KUZIMU 
Siku moja nilikuwa nimetumwa dukani na mama yangu mkubwa, wakati navuka barabara ghafula nikakutana na mtu ana kila kiungo katika mwili wake kikiwa kimoja kimoja , akajitambulisha kwa jina la Lucifer akanipa mkono ila nikakataa, akauchukua mkono wangu kwa nguvu akanikumbatia, nikajikuta chini ya bahari. Akaja mwenyewe  nikaogopa sana akaniambia nimekuchagua kabla hujazaliwa  kwa sababu una akili sana. 
Theresia akiwa anaelezea ushuhuda wa yale aliyaona katika ulimwengu wa kishetani.
Akaniambia nilipozaliwa aliniwinda sana ila alishindwa kunichukua kwa sababu bibi yangu alikuwa ananiombea sana . Lucifer akaniambia anataka niwe mke wa mtoto wake. Tukafunga ndoa  na baada ya miezi 6 baba yake akaniambia anaweza  kunipa nguvu nyingi sana lakini anataka nimtumikie yeye. Baada ya miaka 6 akanipeleka shemu Fulani ndani ya bahari ya pacific lakini ni chini sana, sehemu hiyo ni mji kama ilivyo miji ya huku.
Tukaingia sehemu Fulani tukamkuta dragon ambae alianza kuongea na Lucifer, nikafunga macho na nikajisikia kujawa na  nguvu sana, akaniambia amenipa nguvu na mamlaka ya kumiliki na kutawala fahamu za wanadamu.

Mama mzazi wa Theresia alianza kulia kwa uchungu sana baada ya kunza kusikia habari hizi za kutisha ambazo mwanae wa kuzaa ameyapitia.


Siku moja niliamka asubuhi nikiwa na njaa sana kwa sababu usiku wake sikula chakula, Lucifer akaniambia kuna meli inaitwa Mv spice nikaenda na baadhi ya watu tukatega nyaya za kopa, ile meli ikawa inakuja tukatega pale maji yanapogawanyikia  ili watu waseme ni mkondo wa maji, kuna maneno nikayasema halafu nikasimama pembeni, ile meli ikaanza kuzama mpaka kwenye kina cha chini kabisa cha bahari ambacho nilitaka mimi, kisha  tukaunganisha mabomba mpaka kule pacific na tukapata damu nyingi sana. Mimi nilikuwa nahitaji kunywa damu kiasi cha tani 5000 kwa siku ili niwze kutena kazi kwa nguvu nyingi.

Theresia akiendelea kuelezea huku mama mzazi akiwa anaendela kusikiliza kwa umakini wakiwa na Mchungai Josephat Gwajima

Pia kazi yetu nyingine ilikuwa kuwafanya watu wanaompenda Mungu waache kabisa na kuanza kuwaza vitu vilivyo tofauti kabisa na mapenzi ya Mungu, na waliuwa wakiifanya kazi hii kwa ku-control akili na fikra za wanadamu, yani utawala mkubwa  wa shetani ni kuzishika na kuzikamata fikra za wanadamu ili watende mambo ya kumchukiza Mungu na kujiondolea neema ya Mungu, na walikuwa na uwezo wa kumfanya binadamu atende jambo lolote baya iwe kuuwa,kulewa kutokwenda kanisani.

ULITOKAJE HUKO?
Nakumbuka ilikuwa muda wa kulala huko kuzimu kama kawaida huwa tunalala ila siku hii ikawa tofauti kwa maana nilianza kusikia sauti za watu wanaita njooo njoooo kwa jina la Yesu, mara nikasikia nguvu zinaniishia na nikawa sijielewi kabisa mara nikashanga nimetokea katika viwanja vya tangamano.
Mama yake Theresia anasema kabla ya mtoto wake kurudi alikuwa na matatizo ya kuumwa magojwa yasiyoisha ya kila wakati. Pia alikuwa na tabia ya uvivu na kulala sana , pia hakupenda kusali kabisa, pia kipindi cha mitihani aliugua sana, mama yake Theresia aliongea haya huku akibubujikwa na machozi maana alikuwa hajui kama alikuwa anaishi akiwa na picha picha tu ya mtoto wake na kumbe mtoto halisi alikuwa yuko kuzimu tena ameolewa na shetani na anaifanyia Dunia mambo ya ajabu ya kuiteketeza.
Theresia akimshukuru sana Bwana Yesu kwa kumuokoa na kumrejesha tena katika ulimwengu huu...maana alikiri amekuwa akitafuta ukombozi kwa muda mrefu...

Theresia akiombewa na Mchugaji Kiongozi Josephat Gwajima na Mchungaji Mwandamizi Eng.Yekonia Bihagaze ili kujazwa roho mtakatifu baada ya kuongozwa sala ya toba na kummpokea Yesu kwa Bwana na Mwokozi binafsi wa Maisha yake.

Theresia akiwa amejazwa roho mtakatifu na akinena kwa lugha.
Mchungaji Josephat Gwajima akitoa ufafanuzi.
Shetani anauwezo wa kumuona mtu na maisha yake,vipawa na karama ambazo Mungu amempatia mtu tangu akiwa tumboni mwa mama yake, na ndio maana Theresia alivyofika kuzimu akaambiwa amekuwa akitafutwa siku nyingi sana toka akiwa tumboni ila maombi ya bibi yake yalimkwamisha kuchukuliwa mapema.
Mchungaji Josephat Gwajima akifafanua.
Pia mchungaji Josephat Gwajima aliendelea kuelezea kuhusu kazi hasa aliyoielezea Theresia, Theresia alisema kuwa alikuwa anauwezo wa kuwashikilia fikra, akili na fahamu mwanadamu yeyote..ni hio ndio nguvu hasa ya utawala wa kishetani, kwa lugha nyingine ni typical LUCIFERIC KINGDOM agenda kucheza na mawazo ya wanadamu na kuwapandia mapando ya mawazo ya ajabu ya kutenda dhambi,na ndio roho ya Mpinga Kristo inavyotenda kazi (THE ANTICHRIST)
Mchungaji Josephat Gwajima akiwa anasisitiza kuwa ni lazima kila mtu awe na uwezo wa kuomba na kuishinda roho ya mpinga Kristo na kuushinda ule uwezo wa Shetani wa kumvuvia mtu kufanya maovu, kwa maana shetani ndio anayesababisha mambo yote maovu kufanyika na mwanadamu..

Hapa Mchungaji alikuwa anamaanisha,kwa mfano shetani akiwa anataka kumtumbukiza mtu kwenye ulevu,hawezi akawa anamshushia pombe kutoka mawinguni zimjie alipokaa...bali atamuingizia wazo la kunywa pombe na kumshawishi kuwa anakibali cha kunywa na ndipo mtu mwisho wa siku unamkuta kalala kwenye mitaro kapoteza fahamu kwa ulevi au kafa kabisa...lakini chanzo ni uvuvio wa kishetani kwenye akili ya mwanadamu.

USHAURI ANAOTOA THERESIA KWA WATU WENGINE
Watu inabidi wamtafute Yesu kwa kiwango cha juu sana, kwa sababu yeye ndiye atakayeweza kuwapa kila kitu wanachokihitaji, pia anasema vijana wengi wapo kwenye hatari ya kuangamia hivyo kama hawatamtafuta Mungu hakika wataangamia .

Theresia akiwa anamsifu Mungu kwa Nyimbo kwa maana kuwa kumbe alikuwa anakipaji cha kuimba pia lakini kumbe shetani alikuwa amekifunika.

Pia anamshukuru Mungu kwa kumrudisha kutoka katika vifungo vya shetani maana yeye mwenyewe ilikuwa ni ngumu sana kutoka huko, anachoweza kufanya ni kumtumikia Mungu na kumpenda daima na akaahidi kumuimbia Mungu siku zote kwa kuwa Mungu ndiye mkombozi wake.AMEN 

Tuesday, November 26, 2013

KATIKA SIKU YA PILI YA MKUTANO MKUBWA WA KIHISTORIA TANGA NA MCHUNGAJI JOSEPHAT GWAJIMA

WATU ZAIDI YA KUMI WATOA USHUHUDA WA KUOKOLEWA KUTOKA MSUKULENI

Katika siku ya pili ya Mkutano Mkubwa wa kutokea katika mkoa wa Tanga kumekuwa na matendo makuu na maajbu ambayo Mungu ameyatenda kupitia kwa Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima, wa Kanisa la Glory of Christ (T)  Church- Ufufuo na Uzima.

Mchungaji Josephat Gwajima akiwaombea maelfu ya watu katika uwanja wa Tangamano.

Wakati wa maombezi maelfu ya watu walikuwa wanafunguliwa kwa jinsi ya ajabu kwa jina la Yesu, kutoka katika vifungo vya shetani.

Roho wa Mungu akiendelea kuwafungua watu wa Mungu

Mchungaji Gwajima akiwabariki na kuwawekea ulinzi maelfu ya watu ili wasichukuliwe au kudhuriwa tena na shetani kwa Jina la Yesu

HALIMA ALLY
Anatoa ushuhuda wake na kuelezea kuwa alikuwa amechukuliwa msukule na Bibi mmoja aitwaye  Nyatanga ambaye ni mchawi, na alikuwa amemuweka kwenye shimo kubwa jeusi.
Halima aliendelea kuelezea akiwa na machungu sana huku akilia kutokana na mateso makali na mambo ya kikatili aliyoyaona huko msukuleni, aliuelezea uamti kuwa chakula alichokuwa anakula ni Pumba za mahindi na za mtama...na shughuli yake kubwa ilikuwa ni kutumikishwa mambo ya kichawi na kuwadhuru wanadamu.

Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akiwa na HALIMA ALLY akiwa anatoa ushuhuda wake kwa machungu sana huku akibubujikwa na machozi ya kwikwi.

Mama yake mzazi aliweza kuitwa na kujitokeza na akaelezea kuwa mtoto wake alikuwa hana maendeleo mazuri shuleni wala nyumbani na alikuwa hajui hasa chanzo ni nini.

Mama yake Halima alitoa kauli nzito za kulaani vitendo vya kichawi na akamshukuru sana Mungu kwa kumuokoa mtoto wake kutoka utumwani mwa shetani, na wote wawili walimpokea Yesu na wameahidi kummpa Yesu maisha yao milele yote.

HUSSEIN OMARY
Ni kijana ambaye anaishi Tanga mjini alifika siku ya Pili ya mkutano, maisha yake yalikuwa na mikosi isiyoisha.
Lakini baada ya maombezi ya Mchungaji Josephat Gwajima ikaja kugundulika kuwa nafsi ya  Hussein ilikuwa imechukuliwa msukule kwa njia za kichawi na alikuwa anatumikishwa kulima mashambani huko Bumbuli.


Mchungaji Josephat Gwajima akiwa na Hussein Omari mbele ya maelfu ya watu akiwa anatoa ushuhuda wake.

Mama yake Hussein akilia kwa uchungu huku akielezea furaha yake moyoni kwa kummpata tena mwanae wa mwisho Hussein,Pia Hussein akiwa analia kwa furaha kwa kuweza tena kumuona mama yake Mzazi
Hussein akimshukuru Mungu na kuahidi kumkabidhi bwana Yesu maisha yake milele.

Mama yake mzazi Hussein (mwenye nyekundu) na Mama mdogo katikati wakimlaki mtoto wao baada ya kurudishwa kutoka msukuleni.
MWANAIDI JULIASI

Dada huyu alipokea uponyaji wake baada ya kuombewa na mchungaji Josephat Gwajima kwa Jina la Yesu, ni msichana ambaye kwa muda mwingi ameishi na mama yake wa kambo.

Lakini ikafikia wakati akachukuliwa msukule na huyo huyo mama wa kambo na kuplekwa kutumikishwa katika mashamba, ambapo, yeye mwenyewe anaelezea huku akiwa analia sana kiasi cha kuishiwa nguvu, kuwa alikuwa analimishwa sana kwa njia za kichawi mashamba ambayo ni makubwa sana..

Lakini Baada ya maombezi alianza kusikia sauti ya Mungu inamuita njoo..na ndipo alipoambiwa na huyo mchawi aliyekuwa anamtumikisha kuwa hafai na aondoke mara moja na hatimaye akajishtukia yuko uwanja wa Tangamano.

Mwanaidi Julias akimshukuru Mungu kwa kumuokoa kutoka katika kifungo cha shetani.
KHADIJA KASSIAN
Binti huyu anaitwa Khadija Kassian ni mkazi wa Tanga mjini ametoa ushuhuda wake kuwa alikuwa juu ya mti na kazi yake ilikuwa kumfanyia ushirikina mme wake.

Baada ya maombezi Khadija alikiri kuchukizwa sana na mambo ya kutumikishwa na shetani na alikiri kumkabidhi Yesu Kristo maisha yake.

Alimshukuru sana Mungu kwa kumuokoa.
Khadija Kassian akihojiwa na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima na akikiri mbele za watu kazi alizokuwa anaifanya ya kumufanyia ushirikina mme wake, ila amekiri kuacha na kumpokea Yesu.
Jojina Leonada, ndio jina la huyu dada, alikuwa anamuelezea Mchungaji Josephat Gwajima alipokuwa anamuhoji mbele ya Maelfu ya umati wa watu.Alitoa ushuhuda wake kuwa alikuwa amechukuliwa na Bibi mmoja wa kimakonde, na alikuwa amemuweka nyuma ya mlango chumbani kwa huyo Bibi, ambaye ananyumba yake huko malamba sehemu moja mjini Tanga, aliendelea kutoa shuhuda kuwa alikuwa akifanywa kiti na kukaliwa pindi ambapo bibi huyo alikuwa anaenda kufanya mambo ya kichawi...yani alikuwa chombo cha usafiri kabisa...bibi anamkalia na yeye anaenda, mfano wa punda.


Jojina akiwa anamshukuru Mchungaji Kiongozi kwa kumuombea kwa Jina la Yesu na amerudishwa kutoka msukuleni.


HILDA JOHN
 Ni mwanamke aliyekuwa anaishi mjini Tanga lakini kumbe alikuwa amechukuliwa msukule na bibi yake huko barabara ya 19 ambako alikuwa anatumikishwa mabo mengi ya kichawi

Hilda akiombewa na Mchungaji Kiongozi Josphat Gwajiama.

SIKUZANI MSIAKA
Huyu ni mtoto wa kike mwenye umri wa Miaka 19 anaishi Tanga Barabara ya 16, baada ya kuombewa na Mchungaji Josephat Gwajima katika uwanja wa Tangamano, alianza kutoa ushuhuda wake.
Alisema alikuwa anaishi chini ya Bahari ya Hindi, na huko alikuwa analishwa nyama za watu, alianza kuelezea ilikuwaje hadi akawa huko chini ya bahari na ndipo akasema katika siku ambayo haifahamu vizuri mwaka 2009 alianza kuota ndoto mbaya mbaya sana, na zikaendelea kwa kipindi kirefu sana hadi siku moja akawa anaota ameshikiwa upanga na mkuki akiongozwa aelekee baharini na ndipo alipokuwa hadi anarudishwa uwanjani hapo.
Msichana aitwaye Sikuzani akimuelezea Mchungaji Josphat Gwajima kuhusu maisha yake ya kulishwa nyama za watu chini ya bahari ambako amekuwa huko Tangu mwaka 2009.

Sikuzani alimshukuru Mungu kwa Kumukomboa kutoka katika vifungo vya shetani na aliahidi kumpokea Yesu kuwa Bwana na Muokozi wa Maisha yake.

 Fadhili ni kijana anayeishi Chimbageni katika mkoa wa Tanga, na yeye aliweza kuokolewa baada ya maombezi na mchungaji Josephat Gwajima.

Yeye mwenyewe alishuhudia akisema kuwa alikuwa analimishwa mashamba makubwa sana, na anamfahamu aliyekuwa amamchukua kwa njia za kichawi na kumtumikisha , na akadai kuwa na Mama wa nyumba ya Jirani..

Pia akasema kuna vipindi anapelekwa kishirikina katika msitu mkubwa sana kufanya mambo ya uchawi pia.
Fadhili Chamshama akilia kwa uchungu akiwa anaelezea mateso makalia aliyokuwa anatendewa huko msukuleni

RODGERS FREDERICK
Ni kijana mdogo ambaye na yeye alifanikiwa kuachiwa shetani baada ya maombezi na Mchungaji Josephat Gwajima, Rodgers alipoulizwa aelezee alikuwa wapi akasema alikuwa msikitini alipokuwa amekewa jini maimuna.
Na aliyekuwa amemmpeleka msikitini ni shekh aliyemtambulisha kwa Jina moja la Hassan ambaye ni sheikh kwenye msikiti uliopo mjini Tanga katika barabara ya 15
Rodgers anaelezea jinsi sheikh Hassan alipokuwa anamtumia kupandisha mashetani na kuongea kiarabu, na kumtumia kwenye mambo ya kishirikina

Kijana Rodgers Frederick alimshukuru Mungu kwa Kumuokoa na akaahidi kummpokea Yesu kuwa Bwana na muokozi binafsi wa Maisha yake.


ZAWADI
Anaelezea kuwa alikuwa amechukuliwa msukule na Bibi upande wa Baba yake mzazi, anaendlea kusema kuwa bibi huyo alikuwa anamtuma usiku wa manane akawamwagie watu madawa ambayo yeye anaelezea kuwa zile dawa ni kwa ajili ya kuwapumbaza watu akili, na kuwavurugia maisha.
 Zawadi alipoulizwa kuwa ametoka wapi kwa sasa akasema alikuwa chini ya meza kwenye nyumba ya huyo bibi, ghafla akaanza kusikia sauti inamwita na bibi yakee akaiskia pia akshtuka sana, bibi yake akaanza kumfukuza kwa kumpigia kelele "ondoka! ondoka! usiniletee balaa""!! na yeye akaanza kusikia kwa jina la Yesu Njooo"" na ndipo akazidi kukimbia na akajishtukia yuko katika uwanja wa Tangamano
Zawadi anamshukuru sana Mungu kwa kumkomboa aliahidi kummpokea Yesu na kuanza kumtumikia Mungu.

ANNA RAPHAELI
Kisa cha Anna kinasikitisha na kinafanya kila mtu mwenye akili amlaani shetani, Anna alirudishwa baada ya kuombewa na Mchungaji Josephat Gwajima, Aisema huku akiwa analia kwa uchungu sana na kudai kuwa alikuwa amewekwa kwenye chupa, ambako alikuwa amewekwa kwa ajili ya kuwalea watoto, kwenye hiyo hiyo chupa.
Aliendelea kusema kuwa kwenye chupa kulikuwa na watoto wadogo sana ambao yeye lalifungiwa nao ili awalee, Baada ya maombezi siku hii alianza kuhisi chupa inawaka moto na anahamishwa na sauti ya Mungu iliyokuwa inamuita, huku wale watoto nao wakimuomba aende nao..lakini baada ya kitambo kidogo akajikuta yuko katika uwanja wa Tangamano.

Anna Raphaeli alimshukuru Mungu kwa kumkomboa kutoka kwenye kifungo cha shetani na ameahidi kumpokea Yesu Kristo kuwa Bwana na Muokozi wa Maisha yake.
Ni siku ambayo iliambatana na watu kurudishwa na pia kurudishiwa vyote ambavyo shetani amekuwa akiwadhulumu, kwa jina la Yesu watu wengi wamerudi na kuponywa kabisa.

Mungu amembariki sana Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima kwa kumfikisha katika mikoa ya Arusha, Moshi na sasa ni Tanga na kote huko kumekuwa na miujiza na matendo makuu ya Mungu ambayo yamewafanya watu waokolewe kutoka katika mikono ya shetani.

NI SAA YA UFUFUO NA UZIMA DUNIANI