BINTI AITWAYE THERESIA AMBAYE ALIKUWA ANATUMIKISHWA NA SHETANI AELEZEA JINSI ALIVYOSHIRIKI KATIKA KUIZAMISHA MELI YA MV SPICE HIGHLANDER KWA NJIA ZA KISHETANI.
Theresia ni binti aishiye Jijini Tanga na Mama yake mzazi, na siku hii ambayo alifunguliwa kutoka kuzimu kwa shetani alikuwa amekuja kwenye Mkutano wa Injili uliokuwa umeandaliwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima Jijini Tanga na Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima.
Na baada ya Mchungaji Josephat Gwajima kuanza kuwaombea maelfu ya watu ambao walikuwa mkutanoni wengi walifunguliwa, na waliokuwa katika vifungo vya shetani, na misukuleni walifunguliwa na kurejeshwa katika hali zao za kawaida.
Mchungaji Kiongzoi Josephat Gwajima akiwa na Binti Theresia pamoja na Mama mzazi wa binti Theresia |
Theresia akiwa tayari kuanza kuelezea habari nzima.. |
ALIFIKAJE KUZIMU
Siku moja nilikuwa nimetumwa dukani na mama yangu mkubwa, wakati navuka barabara ghafula nikakutana na mtu ana kila kiungo katika mwili wake kikiwa kimoja kimoja , akajitambulisha kwa jina la Lucifer akanipa mkono ila nikakataa, akauchukua mkono wangu kwa nguvu akanikumbatia, nikajikuta chini ya bahari. Akaja mwenyewe nikaogopa sana akaniambia nimekuchagua kabla hujazaliwa kwa sababu una akili sana.
Theresia akiwa anaelezea ushuhuda wa yale aliyaona katika ulimwengu wa kishetani. |
Akaniambia nilipozaliwa aliniwinda sana ila alishindwa
kunichukua kwa sababu bibi yangu alikuwa ananiombea sana . Lucifer akaniambia
anataka niwe mke wa mtoto wake. Tukafunga ndoa
na baada ya miezi 6 baba yake akaniambia anaweza kunipa nguvu nyingi sana lakini anataka
nimtumikie yeye. Baada ya miaka 6 akanipeleka shemu Fulani ndani ya bahari ya
pacific lakini ni chini sana, sehemu hiyo ni mji kama ilivyo miji ya huku.
Tukaingia sehemu Fulani tukamkuta dragon ambae alianza
kuongea na Lucifer, nikafunga macho na nikajisikia kujawa na nguvu sana, akaniambia amenipa nguvu na
mamlaka ya kumiliki na kutawala fahamu za wanadamu.
Mama mzazi wa Theresia alianza kulia kwa uchungu sana baada ya kunza kusikia habari hizi za kutisha ambazo mwanae wa kuzaa ameyapitia. |
Siku moja niliamka asubuhi nikiwa na njaa sana kwa sababu
usiku wake sikula chakula, Lucifer akaniambia kuna meli inaitwa Mv spice
nikaenda na baadhi ya watu tukatega nyaya za kopa, ile meli ikawa inakuja
tukatega pale maji yanapogawanyikia ili
watu waseme ni mkondo wa maji, kuna maneno nikayasema halafu nikasimama
pembeni, ile meli ikaanza kuzama mpaka kwenye kina cha chini kabisa cha bahari
ambacho nilitaka mimi, kisha tukaunganisha mabomba mpaka kule
pacific na tukapata damu nyingi sana. Mimi nilikuwa nahitaji kunywa damu
kiasi cha tani 5000 kwa siku ili niwze kutena kazi kwa nguvu nyingi.
Theresia akiendelea kuelezea huku mama mzazi akiwa anaendela kusikiliza kwa umakini wakiwa na Mchungai Josephat Gwajima |
Pia kazi yetu nyingine ilikuwa kuwafanya watu wanaompenda
Mungu waache kabisa na kuanza kuwaza vitu vilivyo tofauti kabisa na mapenzi ya
Mungu, na waliuwa wakiifanya kazi hii kwa ku-control akili na fikra za wanadamu, yani utawala mkubwa wa shetani ni kuzishika na kuzikamata fikra za wanadamu ili watende mambo ya kumchukiza Mungu na kujiondolea neema ya Mungu, na walikuwa na uwezo wa kumfanya binadamu atende jambo lolote baya iwe kuuwa,kulewa kutokwenda kanisani.
ULITOKAJE HUKO?
Nakumbuka ilikuwa muda wa kulala huko kuzimu kama kawaida huwa tunalala ila siku hii ikawa tofauti kwa maana nilianza kusikia sauti za watu
wanaita njooo njoooo kwa jina la Yesu, mara nikasikia nguvu zinaniishia na nikawa sijielewi
kabisa mara nikashanga nimetokea katika viwanja vya tangamano.
Mama yake Theresia anasema kabla ya mtoto wake kurudi
alikuwa na matatizo ya kuumwa magojwa yasiyoisha ya kila wakati. Pia alikuwa na
tabia ya uvivu na kulala sana , pia hakupenda kusali kabisa, pia kipindi cha
mitihani aliugua sana, mama yake Theresia aliongea haya huku akibubujikwa na machozi maana alikuwa hajui kama alikuwa anaishi akiwa na picha picha tu ya mtoto wake na kumbe mtoto halisi alikuwa yuko kuzimu tena ameolewa na shetani na anaifanyia Dunia mambo ya ajabu ya kuiteketeza.
Theresia akimshukuru sana Bwana Yesu kwa kumuokoa na kumrejesha tena katika ulimwengu huu...maana alikiri amekuwa akitafuta ukombozi kwa muda mrefu... |
Theresia akiwa amejazwa roho mtakatifu na akinena kwa lugha. |
Mchungaji Josephat Gwajima akitoa ufafanuzi.
Shetani anauwezo wa kumuona mtu na maisha yake,vipawa na karama ambazo Mungu amempatia mtu tangu akiwa tumboni mwa mama yake, na ndio maana Theresia alivyofika kuzimu akaambiwa amekuwa akitafutwa siku nyingi sana toka akiwa tumboni ila maombi ya bibi yake yalimkwamisha kuchukuliwa mapema.
Mchungaji Josephat Gwajima akifafanua. |
USHAURI ANAOTOA THERESIA KWA WATU WENGINE
Watu inabidi wamtafute Yesu kwa kiwango cha juu sana, kwa sababu
yeye ndiye atakayeweza kuwapa kila kitu wanachokihitaji, pia anasema vijana
wengi wapo kwenye hatari ya kuangamia hivyo kama hawatamtafuta Mungu hakika
wataangamia .
Theresia akiwa anamsifu Mungu kwa Nyimbo kwa maana kuwa kumbe alikuwa anakipaji cha kuimba pia lakini kumbe shetani alikuwa amekifunika. |
Mungu anaweza asante Yesu huu ushuhuda unatufundisha vitu vikubwa ving sana,kumbe shetana naye aweza kukufahamu toka ukiwa tumboni ,Mwenyenzi Mungu atuongoze kwani waweza mwona mtu anatabia fulani za ajabu unamlaumu kumbe siyo yeye
ReplyDeleteAmina majeshi ya Bwana
ReplyDelete