Wednesday, December 18, 2013

MCHAWI ANASWA KATIKA MKUTANO WA UFUFUO NA UZIMA MOROGORO


Ikiwa ni siku ya tatu ya mkutano wa ufufuo na uzima unaoendelea katika viwanja vya vya shule ya sekondari ya morogoro mchawi mmoja aliyejulikana kwa jina la Fatuma amekamatwa katika mkutano huo akiwa yuko katika shughuli zake za kila siku za kichawi.

Dada huyo aliyekamatwa na Nguvu za Mungu alielezea akasema alikuwa na wenzake ambao walitumwa na bosi wao ambaye ni mchawi na mganga wa kienyeji maarufu kutoka mjini Bagamoyo wilaya ya pwani kuja katika mji wa Morogoro kuchukua miili ya watu waliokufa katika nyumba za kuhifadhia maiti za hospitali(mochuari) kwa ajili ya kitoweo.

Akizungumza alisema yeye na wenzake walipoteana walipofika karibu na hospitali ya rufaa ya mji wa Morogoro ambapo ni eneo la jirani na sehemu mkutano unapofanyika, alipofika maeneo hayo alisikia nguvu inamvuta kwa nguvu na kumpeleka asipotaka yeye ndipo alipojikuta ametua katika viwanja shule ya sekondari ya Morogoro ambapo ndipo mkutano unapofanyika
Dada huyo aliyeonekana kuwa na wasi wasi alisema tulikuja mimi na wenzangu kwa usafiri wa njia ya fisi lakini tulipokaribia hospitali sijui nini kimetokea na mimi nikasikia nguvu zinanivuta nikajikuta niko mahali hapa

ALIANZAJE UCHAWI

Akielezea jinsi alivyoanza uchawi alisema miaka kumi na tano iliyopita alikua anaumwa ndipo alipoamua kuondoka kwao Babati(Manyara) kwenda kutibiwa mkoani Pwani kwa mganga aliyejulikana kwa jina la Idi. Alipofika kwa mganga aliambiwa akachume pilini dawa Fulani na aitafune, alipofanya sawasawa na maelekezo ya yule mganga ndipo alipojiona anaanza kuingiwa na ukatili usiokuwa wa kawaida na akaanza kupata hamu ya kula wanadamu wenzake, kuanzia siku hiyo ndipo alipoanza kuagizwa na Idi kwa ajili ya kufanya shughuli za kichawi pamoja na wenzake.

NAMNA ALIVYOKUWA AKITENDA KAZI

Yeye na wenzake walikuwa wanawashughulikia hasa watu ambao waliokoka na baada ya hapo wakarudi nyuma, akieleza jinsi walivyokua wakiifanya kazi hiyo alisema mtu yeyote aliyewahi kuokoka na baada ya hapo kumuacha Yesu anakuwa na majini mawili wanaotumwa kukaa ndani yake, na wachawi hawa wanapomfuata mtu huyo wanaongea nayale mapepo na wanayaagiza yamnyonge mtu huyo na mtu huyo anakufa mara moja

Katika utendaji kazi wake yeye ndiye aliyekuwa kiongozi wa kikundi chake hicho walichokuwa wanatenda shughuli hizo za kichawi.Alisema mimi niliwekwa kuwa kiongozi wa wenzangu kwasababu mimi nilikua nimefanikiwa kuwaua watu watatu waliokua wameokoka na kurudi nyuma. Kule kwenye uchawi mtu aliyefanikiwa kuwaua watu waliorudi nyuma ndie anakua na cheo kuliko wengine, mimi niliua watu ambao walikua hawajawahi kuokoka zaidi ya thelathini na waliokua wameokoka na kurudi nyuma watatu alisema dada huyo.

Akielezea alisema sisi tulikuwa na uwezo wa kuwaua watu kwa matukio tuliyokua tunayatengeneza, unaweza ukakuta mtu anatembea njiani alafu akawa kama ameumwa na nyoka lakini nyoka mwenyewe hamuoni, mtu huyo baada ya masaa machache atakufa na sababu itakuwa kwamba aliumwa na nyoka lakini sivyo tunakuwa ni sisi tumemtengenezea kifo ili tukamle nyama.

WATU ALIOWAHI KUWAUA

Alisema anakumbuka miaka mitano iliyopita alimuua mdogo wake aaliyekuwa anajulikana kwa jina la Udiyomboli, watu watatu ambao waliwahi kuokoka na kasha kurudi nyuma pamoja na wengine Zaidi ya thelathini aliowaangamiza kwa kutumia uchawi
Baada ya hapo dada huyo akiongea kwa huzuni aliomba msaada akasema, nimechoka kufanya uchawi siyapendi maisha haya na sitaki tena kurudi kule Bagamoyo.

Dada huyo tayari ameshaachana na mambo ya uchawi na amempokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa maisha yake.

No comments:

Post a Comment