Sunday, October 6, 2013

MISUKULE YARUDISHWA MKUTANO WA MCH. JOSEPHAT GWAJIMA JIJINI ARUSHA

Ni wiki moja sasa tangu mkutano Mkubwa wa Injili unaoongozwa na Kanisa la Ufufuo na Uzima kuanza jijini Arusha na leo ikiwa ni hitimisho lake. Mkutano uliovuta hisia na macho ya watu wengi kwa kile wasichokifahamu kuwa Yesu Kristo anaweza kufufua mtu ambaye awali alidhaniwa kuwa amekufa.

Miujiza Mingi imefanyika tangu kuanza kwa mkutano huo lakini hapa tunakuletea shuhuda chache za watu ambao walikuwa wamechukuliwa msukule, wengine kufa kabisa na kurudishwa kupitia mkono wa Mchungaji Josephat Gwajima. Kumbuka kuna watu wengi wamerudishwa na kuwekwa huru hawa wachache wameandikwa ili ujue kuwa Yesu Kristo bado anatenda kazi duniani leo.

Mchungaji Josephat Gwajima akimhoji dada Grace,
Mara baada ya Kurudishwa kutoka msukuleni
Grace akiwa amejishika kichwa baada ya kurudishwa

Dada Grace akihojiwa na mtu wa
Information Ministry




Huyu ni dada Grace alichukuliwa msukule na kupelekwa Singida; alipohojiwa alisema kuwa alichukuliwa na mwanamke mmoja aitwaye Farida.

Mara ya mwisho anakumbuka kuwa alichukuliwa akiwa anajifungua Hospitali ya Mount Meru, ndugu zake waliambiwa kuwa mtoto amefia tumboni na hapo akajikuta yupo Singida bila kujua kinachoendelea baadaye.

Aliendelea kusimulia kuwa wakati watu wanaomba huku yeye kule msukuleni alisikia sauti ikimwita "Njoo Njoo Grace" 

Grace amefunguliwa na kuwekwa huru kabisa, Uweza wa Mungu ni mkuu kuliko mioyo yetu.




                  ******************************************************************


Mch. Gwajima akimwombea amuone aliyemchukua
msukule


Huyu dada alichukuliwa na kuwekwa msituni, Kilimanjaro. Wakati anahojiwa na Mch. Gwajima alisema kuwa hamkumbuki aliyempeleka huko; ndipo Mchungaji Gwajima akamwombea ili amuone, akamwona dada mmoja jirani yake anaitwa Jane ambaye aliwachukua wote wawili yeye na mumewe.

Akiongea kwa machozi na kulia alisema kuwa Mumewe amemwacha huko, na kumwacha hana msaada.

Ushuhuda huo uliovuta hisia za watu, uliishia kwa kuomba Mch. Gwajima amsaidie kumwokoa mumewe ambaye amewekwa kwenye chungu huko msukuleni alipokuwa.

Mchungaji Gwajima aliamuru Mumewe arudi katika Jina la Yesu Kristo.


No comments:

Post a Comment