Thursday, October 24, 2013

WALIOKUWA VIWETE ZAIDI YA SABA WATEMBEA BAADA YA MAOMBEZI MKUTANO WA UFUFUO NA UZIMA - MOSHI NA Mch. Josephat Gwajima

MIUJIZA NA MAAJABU AMBAYO MUNGU ANAENDLEA KUWATENDEA MAELFU YA WAKAZI WA MOSHI SIKU YA JUMATANO TAREHE 23.10.2013 KUPITIA KWA MCHUNGAJI KIONGOZI WA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA JOSEPHAT GWAJIMA, KATIKA MKUTANO MKUBWA WA INJILI WA KANISA LA UFUFUO NA UZIMA,


Mchungaji Kiongozi, wa Kanisa la Glory of Christ (T) Church - Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima, lenye makao yake makuu Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Tanganyika Packers - Kawe , ambaye Mungu amchagua na kumpaka mafuta na  sasa anaongoza Mikutano mikubwa ya Injili kuzunguka nchi yote ya Tanzania. Baada ya kutoka Jijini Arusha na sasa yuko mjini moshi na maelfu ya watenda kazi, ambako kumekuwa na muitikio mkubwa ambao haujawai kutokea mjini Moshi kwa maelfu na maelfu ya wananchi kufika katika viwanja vya mashujaa kwa ajili ya kusikiliza neno la Mungu, kummpokea Yesu na kuponywa kutoka katika vifungo na shida ziletwazo na shetani.


Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima (wa pili kutoka kushoto), akiwa na Mchungaji mwandamizi (wa kwanza kushoto) Mchungaji Mwangasa, wakiwa na baadhi ya wananchi wa Mjini Moshi ambao wameweza kufunguliwa kutoka katika kifungo cha ulemavu wa muda mrefu katika Mkutano wa mkubwa wa Injili unaoendelea katika uwanja wa mashujaa mjini Moshi, Pichani wakiwa  na nyuso za furaha , wakiwa wamenyanyua magongo , wakimshukuru Mungu kwa kuwafungua kutoka katika kifungo cha shetani.
Anayehojiwa ni Mama Petronila Andrew mwenye umri wa miaka 70, ambaye alikuwa hawezi kabisa kutembea, kutokana na kusagika kwa mifupa yake ya kiuno na miguu kusagika lakini ameelezea ni jinsi alivyoskia hali yake inabadilika na maumivu kuondoka kabisa wakati ambapo mchungaji kiongozi Josephat Gwajima alipokuwa akifanya maombezi kwa watu wenye magonjwa mbalimbali kuponywa kwa Jina la Yesu.


    Mama Sarapina na Petronila wakiwa katika nyuso za kumshukuru Mungu kwa kuwatendea muujiza na kuwaponya magonjwa yao ya ulemavu.


Ministrial Pastor, Sofia amabye ni moja kati ya maelfu ya watenda kazi wa kanisa la ufufuo na uzima akiwa anamuongoza mama ambaye aliweza kutembea na kufunguliwa baada ya maombezi ya Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima.


    Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima akiwa amenyanyua yaliyokuwa magongo ya Kijana Gervas, mwenye umri wa miaka 23, alipooza miguu kwa muda wa miaka 3. Kijana  Gervas alionekana akiwa na mshangao alivyoweza kutembea  na kuamua kumpa Yesu maisha yake baada ya kamponya na magonjwa yake pamoja na madhaifu.


Mchungaji Mwandamizi, Bryson Lema ambaye ni mchungaji mwandamizi wa Mchungaji kiongozi Josephat Gwajima, baada ya kumuombea na kumuweka huru, Mama mkazi wa Mjini Moshi ambaye alifika katika viwanja vya mashujaa kwa ajili ya kupokea muujiza wake na hatimy kuponywa kabisa tatizo lak la miguu.
Mchungaji Kiongozi, Jospehat Gwajima akiwa na Messe Shirima mwenye umri wa miaka 38, ambaye shetani amemtesa kwa kuwa na miguu isiyotembea sawa sawa bila ya kuwa na magongo, na pia amehangaika sana mahospitalini lakini alikuwa anapewa matumaini ya kuendelea kutumia magongo, mpaka siku ya tarehe 23.10.2013 ambako Mchungaji Jospehat Gwajima alipomuombea kwa jina la Yesu na akapona magonjwa  na udhaifu wote uliokuwa unamsumbua.






Maelfu ya wakazi wa mjini Moshi wakifuatilia kwa umakini mkutano.


    Mama huyu anaitwa  SARAPIA, ana umri wa miaka 70, amekuwa akisumbuliwa na miguu iliyompelekea kushindwa kutembea kwa muda wa miaka 20, alikiri kuwa baada ya maombezi ya mchungaji kiongozi, amepokea uponyaji na hana maumivi tena.
Mama huyu anamshukuru Mungu kwa kumponya, alimpokea Bwana Yesu na ameahidi kumtumikia Mungu kwa siku zote za maisha yake zilizobakia.


    Mchungaji Kiongozi, Josephat Gwajima akiwa na Mkazi wa Moshi aitwaye Martha mwenye umri wa miaka36, alitoa ushuhuda kuwa,  alikuwa akisumbuliwa na tatizo la miguu kuvimba na kuumwa kiuno kwa muda mrefu sana, jambo lililosababishwa na ajali ya pikipiki,  alishindwa kujizui kububujikwa na machozi mbele ya umati wa watu mara baada ya kupokea uponyaji wake. Alishuhudia mbele ya watu wote kiwa madhabahuni kuwa ameteswa na tatizo hili kwa muda mrefu sana,pia amekuwa ana kwenda hospitalini mara kwa mara bila mafanikio yoyote. Sifa apewe Bwana Yesu amabye pia alimkiri kuwa ni Bwana na mwokozi wa maisha yake na akammpokea.



Mchungaji Mwandamizi, Maxmillian Machumu (kushoto) wa Kanisa la Ufufuo na Uzima akiwa ameyashikilia yaliyokuwa magongo ya Mama Sarapina ambaye ameponywa baada ya maombezi ya Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima katika uwanja wa mashujaa mjini moshi.
Mchungaji Kiongozi Josephat Gwajima akiwaombea baraka na uponyaji maelfu ya wakazi wa mjini moshi waliohudhuria siku ya nne ya mkutano tarehe 23.10.2013 Jumatano, wakazi wa mji wa Moshi wameupokea ujio huu wa mchungaji Gwajima kwa mikono miwili na wanaonesha kiu kubwa ya kuendelea kumjua Mungu na kumtii ili kuzishinda hila zote za shetani na kujiweka huru kutoka katika shida mbalimbali zinazowakabili katika maisha yao.

No comments:

Post a Comment